Blog ya pekee kwa habari uzipendazo

Saturday, November 14, 2015

Kashfa ya ngono yamtesa Benzema



Kashfa ya ngono inayomkabili mshambuliaji wa Ufaransa,Karim Benzena inaweza kumkosesha nafasi ya kucheza fainali za Ulaya mwakani

     

                          Mshambuliaji wa Ufaransa na klabu ya Madrid Karim Benzema

Fainali hizo zitafanyika Ufaransa ambako Benzema anakabiliwa na hatari ya kuzikosa zikifanyika katika ardhi ya nyumbani

Endapo hilo litatokea pigo kwa Ufaransa na mshambuliaji wa Real Madrid
Ushahidi wa mkanda wa video umeonesha kuwa Benzema alificha ukweli wa tukio la yeye kuhusika katika mapenzi na msichana mwenye umri mdogo

Lakini mazungumzo baina yake na mshambuliaji mwenzakeMathieu Valbuena yaliyorekodiwa kwa njia ya simu yake yameonesha kuhusika kwa mshambuliaje huyo

Kwa upande wake Benzema amekuwa akikana kuhusika na kashfa hiyo akieleza kuwa alikuwa akimshauri Valbuena nini chakufanya anapokuwa katika wakati mgumu

Hata hivyo uchunguzi wa polosi unaonesha kuwa Benzema alificha ukweli kuhusu tukio hilo kwa kutoa hongo

Mshikemshike Burundi



Hali ya wasiwasi imezidi kutanda miongoni mwa wananchi wa Burundi kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo uku umoja wa mataifa (UN) ikitafakari kutuma vikosi vyake nchini humo 
                                     Image result for nkurunziza pictures
                                             Rais wa Burundi Pieri Nkurunziza

Balaza la usalama la umoja wa mataifa (UN) limepitisha azimio la kukomesha ghasia nchini Burundi na kufanyika mazungumzo pande kwa mbili zinazohasimiana ili kurejesha hali ya Amani na utulivu
Baadhi ya jumuiya za kimataifa zimeanza kuondoa wafanyakazi wake nchini humo kwa madai ya kuzuka kwa machafuko Zaidi ambayo yamesababisha raia  kupoteza maisha na wengine kukimbilia katika nchi jirani

Baraza hilo limeitishia nchi nhiyo kuiwekea vikwazo na kutuma vikosi vya kulinda usalama nchini humo 

Azimio hilo limepitishwa huku ghasia zikiendelea Burundi hata baada ya Rais Piere Nkurunziza kurejea madarakani kwa muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo
                                              Image result for burundi citizens pictures
                                                    
                                                            Raia wa Burundi

Azimio hilo linamtaka katibu mkuu wa UN, Ban ki Moon kuwasilisha njia mbalimbali kwa baraza hilo za kusaidia kumaliza mzozo wa Burundi katika  kipindi cha siku 15 zijazo

Zaidi ya watu 240 wameuawa na wengine 200,000 wakikimbilia katika nchi za jirani ikiwemo Tanzania tangu kuanza  kwa machufuko hayo aprili  mwaka huu 

Machafuko hayo yalianza baada ya Rais Nkurunziza kutangaza azma yake ya kuwania urais wan chi hiyo kwa muhula wa tatu
      
                                                  Raia wa nchini Burundi

Serikali ya Rais Nkurunziza imekuwa ikikosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa kutokana na kuendelea kwa machafuko hayo huku baadhi ya mataifa yakionesha wasiwasi wa kujirudia kwa mauaji ya kiraia.

Friday, November 13, 2015

Dr Magufuli kutinga uwanjani kesho katika mechi ya Taifa Stars dhidi ya Algeria



 Rais mpya wa Tanzania, John Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya Taifa Stars dhidi ya Algeria keshokutwa, imeelezwa.
                        
  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli

Mechi hiyo ya kwanza ya kusaka timu itakayotinga hatua ya makundi matano kuwania kupata timu tano za Afrika zitakazofuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, aliwaambia waandishi wa habari jijini jana kuwa Rais amepanga kuwa miongoni mwa watu watakaohudhuria kwenye Uwanja wa Taifa siku hiyo kuishuhudia mechi hiyo ya kwanza ya kimataifa kuchezwa kwenye uwanja huo tangu ashike madaraka hayo makubwa.

"Kama hakutakuwa na mabadiliko, Rais Magufuli atakuwapo uwanjani kuwapa sapoti wachezaji wetu wa timu ya taifa ili wafanye vizuri katika mchezo wao dhidi ya Algeria," alisema Sadiki.

Alisema anatumaini nyota wa Stars hawatamuangusha Rais Magufuli siku hiyo kutokana na maandalizi waliyofanya wakiwa kambini Afrika Kusini.

Sadiki pia aliwapongeza washambulia wa Stars, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa kuisaidia klabu yao ya TP Mazembe kutwaa taji la tano la Klabu Bingwa Afrika Jumapili iliyopita.

Jumatatu Stars itasafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Novemba 17 nchini humo.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya  Dar es Salaam limesema litaimarisha ulinzi na usalama wakati wa mechi ya keshokutwa.

Suleiman Kova, Kamada wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, aliwaambia waandishi wa habari jijini  kuwa wamejipanga kuhakikisha mashabiki wanaangalia mechi hiyo kwa amani na utulivu.